Mwakilishi Mkazi wa shirika la linaloshughulika na masuala ya Afya ya Uzazi na  Uzazi wa mpango kwa Wanawake na Wasichana  la EngenderHealth Richard Killian( katikati) akizungumza na Waziri wa Afya ,Maendeleo ya Jamii,jinsia,Wazee na Watoto mapema leo kwenye ofisi ya waziri huyo,Kushoto ni Rais na Mkurugenzi mtendaji wa Shirika hilo bi. Ulla Muller na kulia ni Waziri Ummy Mwalimu.

Rais na Mkurugenzi wa EngenderHealth Bi. Ulla Muller (wa kwanza kushoto) akifafanua jambo wakati alipomtembelea waziri wa afya na kuzungumza mikakati yao katika upande wa afya,rais huyo atatembelea Mkoa wa Manyar.

Waziri wa Afya ,Maendeleo ya jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Ummy mwalimu akiongea na Rais pamoja na Mwakilishi mkazi wa Shirika la EngenderHealth walipomtembelea ofisini kwakwe. Waziri Ummy amesema hivi sasa asilimia 27 ya wanawake wa Kitanzania ndio wanaotumia njia za uzazi wa mpango ambapo serikali ilijiwekea malengo mwaka 2012 kwamba ifikapo mwaka 2020 ifikie asilimia 50 ya matumizi ya njia ya uzazi wa mpango( Picha na Wizara ya Afya).

Feature News & Events

Go to top