Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia , Wazee na Watoto Mh. Dkt. Hamisi Kigwangalla amemuagiza Mkemia Mkuu wa Serikali Prof. Samwel  Manyele kuendelea na uchunguzi wa kimaabara zidi ya vilainishi vilivyo sokoni ili kubaini bidhaa za vilainishi halisi na visivyokidhi viwango na ubora.

Akizungumza hayo kwenye mkutano wake na waandishi wa habari jijini Dar es salaam leo Dkt. Kigwangalla amesema kuwa Mkemia Mkuu wa Serikali hana budi kuendeleza uchunguzi wa kimaabara ili kubaini vilainishi visivyo na kiwango.

“Tunapiga marufuku uuzaji wa vilainishi vya kupima unaofanyika mtaani na sokoni kwa sababu vifungashio vya vilainishi hivyo havikidhi ubora” alisema Dkt. Kigwangalla.

Aidha Dkt. Kigwangalla amesema kuwa marufuku kuingiza vilainishi vilivyotumika (recycled lubricants) visivyo kuwa ubora nchini kinyume cha matakwa ya sheria.


Kwa mujibu wa Dkt. Kigwangalla amesema kuwa asilimia 50 ya vilainishi vya injini, aina ya petroli zilizochunguzwa zilionekana kutokikidhi viwango vya ubora vya vilainishi vya kitaifa.

Kwa upande wake Mkemia Mkuu wa Serikali Prof. Samwel  Manyele amesema kuwa amepokea agizo la Naibu Waziri na amesema kuwa  uchunguzi wa kimaabara wa sampuli za vilainishi zinazoingizwa nchini unafanyika na unaendelea

Aidha Prof. Manyele amesema kuwa mpaka sasa wamesajili  kampuni 28 za kuingiza vilainishi nchini na wameimarisha  ukaguzi wa mizigo ya vilainishi katika viwanda, bandari, bandari kavu, mipaka na viwanja vya ndege.

Kwa mujibu wa Profesa Manyele amesema miongoni mwa vilainishi hivyo ni pamoja na na vilainishi vya injini ikiwemo Oil, Petroli,  Diesel na Gear Oili.

Mkemia Mkuu wa Serikali amebainisha kuwa Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali Nchini iliingiza Vilainishi kuanzia 2013  hadi sasa 2016  na kufanyiwa uchunguzi wa kimaabara na uchunguzi wa ulibaini        Asilimia 50 ya vilainishi vya injini, aina ya petroli zilizochunguzwa zilionekana kutokikidhi viwango vya ubora vya vilainishi vya kitaifa.

“Asilimia 52.6 ya vilainishi vya injini, aina ya Diesel zilizochunguzwa zilionekana kutokikidhi viwango vya ubora vya vilainishi vya kitaifa.

Asilimia 77.7 ya vilainishi aina ya Automobile Transmission Fluids (ATF) zilizochunguzwa zilionekana kutokikidhi viwango vya ubora vya vilainishi vya kitaifa na Asilimia 50.6 ya vilainishi aina ya “Gear oil” zilizochunguzwa zilionekana kutokikidhi viwango vya ubora vya vilainishi vya kitaifa” alimalizia.

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia , Wazee na Watoto Mh. Dkt. Hamisi Kigwangalla akifafanua jambo wakati wa mkutano huo wa kutoa maagizo kwa Mkemia Mkuu wa Serikali juu ya kufuatilia vilainishi . Kushoto kwake ni Mkemia Mkuu wa Serikali Prof. Samwel  Manyele.Mkemia Mkuu wa Serikali Prof. Samwel  Manyele (kushoto) akitoa ufafanuzi wakati wa kupewa maagizo hayo na Naibu Waziri wa Afya Dk.Kigwangalla (katikati). Kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa wizara ya Afya, Dk. Mohammed Ali .

Feature News & Events

Go to top