Customer Feedback Centre

Ministry of Health

IMARISHENI MIFUMO YA UPATIKANAJI NA USIMAMIZI WA UTOAJI WA HUDUMA ZA CHANJO

Posted on: April 23rd, 2024



Katibu Tawala Mkoa wa Njombe ametoa wito kwa wataalamu wa afya kuimarisha Upatikanaji na usimamizi wa huduma za Chanjo na Kutoa majibu ya kitaaluma ili kuepusha taarifa za upotoshaji .

Ameyasema Leo Aprili 23, 2024 wakati akizindua rasmi zoezi la utoaji wa Dozi moja ya chanjo ya HPV dhidi ya saratani ya Mlango wa kizazi kwa Wasichana wenye umri wa miaka 9 hadi 14 katika viwanja vya kituo cha Afya Uwemba, Mkoani Njombe.

"Madhumuni ya wiki hii ni Kutoa Dozi moja ya Chanjo dhidi ya saratani ya mlango WA kizazi (HPV) kwa kiwango cha asilimia 80 kwa wasichana wenye umri wa Miaka 9 hadi 14 wakati wa maadhimisho ya wiki ya Chanjo Afrika.Wiki hii ya Chanjo itaimarisha zaidi utoaji wa chanjo ya HPV sambamba na utoaji wa chanjo zingine zote" amesema Bi. Judica

"Chanjo ya HPV ni chanjo inayotumika kwa ajili ya Kutoa kinga dhidi ya virusi vya Human Papilloma(HPV) vinavyosababisha saratani za Aina mbalimbali ikiwemo saratani ya mlango wa kizazi kwa wakina mama na hovyo kupunguza vifo vitokanavyo na saratani ya mlango wa kizazi" amesema Bi judica

Aidha, Bi judica ameeleza sababu za mabadiliko ya ratiba ya Chanjo ya HPV kutoka Dozi mbili kwenda Dozi moja ni kwamba tafiti za kisayansi zimethibitisha kuwa Dozi moja ya chanjo ya HPV inatosha Kutoa kinga kamili dhidi ya maambukizi ya virusi vinavyo sababisha saratani ya mlango wa kizazi.

Bi. Judica amewahimiza wananchi kujitokeza kushiriki maadhimisho haya, kwa kila mzazi au mlezi Kuhakikisha walengwa wanapata chanjo, lakini pia Kuhakikisha unamtaarifu jirani, ndugu, jamaa au rafiki yoyote unayemfahamu kama ana mlengwa ili aweze kujitokeza kunufaika na huduma za chanjo zitolewazo kupitia maadhimisho haya.

"Mtoto asiyepata Chanjo ni hatari kwa maisha Yake na kwa jamii inayomzunguka kwani anaweza kuambukizwa au kuwaambukiza wengine ugonjwa kwa kutokuwa na kINGA. Hivyo ni jukumu la kila mmoja wetu Kuhakikisha anakuwa mlinzi wa mwenzake" amesema Bi. Judica